Friday, January 4, 2013

IBADA YA KUMUAGA MWANAHABARI FREDDY MTOI LONDON YAGEUKA WASIFU WA MAISHA YAKE

“Alikua mfano dhahiri wa neno mtanashati”
-Zawadi Machibya wa BBC Swahili
Coffin bearers file past-2
Jeneza likitolewa kanisani baada ya ibada.
Kanisa la St Annes Lutheran katikati ya jiji la London juzi Jumamosi lilikuwa kituo maalum cha kumwaga na kuwa wasifu wa maisha ya marehemu Freddy Alex Mtoi aliyekuwa mtangazaji wa BBC Swahili kwa miaka mingi.
Ibada hiyo iliyoendeshwa na wachungaji Tumaini Kalaghe na Mathew Jutta, ilihudhuriwa na wanahabari mbalimbali kutoka BBC , Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania, Clement Kiondo, marafiki wa karibu waliomjua marehemu na wanananchi wa sehemu toka Tanzania, Afrika na Ulaya.
Church entrance-built in 1680
Mratibu wa mazishi , Zawadi Machibya, ambaye ni mtangazaji wa BBC, aliendesha shughuli na kuwajulisha wasemaji wote waliozungumzia kwa kuanza kueleza namna neno “mtanashati” lilivyomvaa na kumfaa Freddy Mtoi aliyefariki usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe 17 Novemba, 2012.
St Annes Church-notice board-1
Mchungaji Mathew Jutta alikumbusha kwamba safari yetu wanadamu huanzia kwa Mungu na kuishia kwa Mungu. Akailinganisha nsafari hiyo na ile ya kutoka nyumbani Afrika kuja Majuu (palipoitwa Mtoni enzi mchungaji alipokuja Ulaya takribani miaka 20 iliyopita). “Kwa wanaobakia ni huzuni lakini kwa anayesafiri ni furaha yenye matumaini.” Akimzungumzia marehemu alitaka zaidi kututuliza roho tuliyobakia.
Coffin-Mourners show last respect
Kutoa heshima za mwisho
Maneno haya yalisimama dede kama kijiti cha dhamira kuu ya msiba. Kwamba badala ya kuhuzunika tujiratayarishe tunakokwenda kwa kuzingatia maneno ya Biblia, Yohana Mtakatifu 3:20 : “ Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.”
Coffin- females sing past
Maombolezo yakiongozwa na kina dada waliokuwa wakiimba kwa nguvu na hamasa.
Wafanyakazi wenzake marehemu Mtoi nao waliendeleza hoja kwa kutueleza undani wa bidii yake marehemu kazini, tabia yake ya uungwana na upole. Akifafanua kwa kina, mtangazaji wa BBC toka Kenya Solomon Mugera alitoa mfano namna marehemu alipokuwa tayari kumenyeka hata wakati wenzake wakitaka kupumzika kama wakati wa sikukuu ya Krismasi. Mugera :“ Marehemu hakuwa mlalamishi au mbishi. Hakuogopa kujaribu kufanya kitu ambacho hakifahamu.”
Freddy Mtoi- Model pic by Seif Kabelele blog
Marehemu. Enzi zake, aling’ara…na ataendelea kung’aara.
(more…)
Read Full Post »
Idhaa ya Kiswahili ya BBC London inawaarifu wapenzi wa BBC, ndugu, jamaa na marafiki hasa walioko Uingereza kuwa, ibada ya kumuaga mtangazaji wake Fred Mtoi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe 17 Novemba 2012 itakuwa Jumamosi tarehe Mosi Disemba 2012.
Ibada hiyo itafanyika katika Kanisa la St. Anne’s Lutheran mjini London kuanzia saa tano kamili asubuhi.
Anuani ya Kanisa ni: St Anne’s Lutheran Church, Gresham Street, London, EC2V.


Marehem anaongelewa vizuri sana na kila aliyemjua au aliyemsikia akitangaza redioni
Safari ya kuupeleka mwili wa marehemu Dar es salaam nchini Tanzania itakuwa Jumatatu tarehe 3 Disemba 2012 jioni kwa ndege ya Shirika la British Airways.
Mwili unatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jumanne saa moja asubuhi.
Mipango ya Ibada na mazishi nchini Tanzania inafanyika nyumbani kwa wazazi wake Tabata Maduka Manne jijini Dar es salaam. Ibada ya kumuaga Fred itafanyika katika kanisa la Lutheran Tabata Kuu saa saba mchana siku ya Jumatano tarehe 5 Disemba 2012. Maziko yatafanyika katika makaburi ya Kinondoni Dar es salaam saa tisa alasiri.
Fred alianza kazi ya utangazaji Radio Tanzania kabla ya kuja Ulaya kwa masomo. Amekuwa akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya shahada ya pili ya Uzamili kuhusu ‘Digital Media’ katika chuo kikuu kimoja cha London.
Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.


Marehemu Freddy Mtoi (kulia) akimhoji mwanamuziki Temba mwaka jana alipoitembelea Uingereza- picha na Urban Pulse

Alishiriki piya katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na aliyepatana na wote. Alikuwa mtangazaji mtulivu na akishikilia kazi alihakikisha anaimaliza vema.
Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.
Fred atakumbukwa kwa umahiri wake katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Shukran za dhati kwa Shirika la BBC kwa kushughulikia na kugharamia mipango yote ya kuusafirisha mwili wa marehemu Fred hadi Tanzania.
Pia shukran kwa wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha mipango ya yote kuhusu msiba huu. Imetolewa na:
Zawadi Machibya
Mratibu wa Mazishi
Idhaa ya Kiswahili ya BBC
London
Kwa maelezo zaidi piga simu
+44 795 260 7038

No comments:

Post a Comment

POSTED STORIES

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...